Job 38:8-13


8 a“Ni nani aliyeifungia bahari milango
ilipopasuka kutoka tumbo,

9 bnilipoyafanya mawingu kuwa vazi lake,
na kuyafungia katika giza nene,

10 cnilipoamuru mipaka yake,
na kuiweka milango yake na makomeo mahali pake,

11 dniliposema, ‘Unaweza kufika mpaka hapa wala si zaidi;
hapa ndipo mawimbi yako yenye kiburi yatakapokomea’?


12 e“Umepata kuiamrisha asubuhi ipambazuke,
au kuyaonyesha mapambazuko mahali pake,

13 yapate kushika miisho ya dunia,
na kuwakung’uta waovu waliomo?
Copyright information for SwhKC